Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 15, 2014

Diaspora, Serikali kujadili maendeleo katika kongamano


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza alipokutana nao mjini London kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini humo, mwishoni mwa wiki. Picha na PMO      
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
London. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali inaandaa kongamano la siku mbili litakalojadili mustakabali wa Watanzania kutoka nchi zote duniani ikiwa ni pamoja na kukutanisha kampuni na wafanyabiashara mbalimbali.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokutana na Watanzania wanaoishi Uingereza kwenye mkutano uliofanyika katika ubalozi wa Tanzania jijini hapa.
Waziri Mkuu alisema kongamano hilo limepangwa kufanyika Agosti 14-15, mwaka huu, linalenga kuitambulisha rasmi diaspora ama jamii ya Watanzania inayoishi ughaibuni kama wadau muhimu katika kuleta maendeleo nchini Tanzania
“Lengo letu hasa ni kutaka jamii ya Watanzania ielewe kwamba tunao Watanzania walioko nje ya nchi kwa maelfu na kuna sehemu mnaweza kuchangia katika maendeleo ya nchi,” alisema.
Mbali na hilo, Waziri Mkuu alisema katika kuitambua rasmi jamii ya wanadiaspora, Serikali itapenda kujua wako wangapi na wanafanya nini ili kama Serikali itahitaji ujuzi/utaalamu wao inaweza kuwapata wapi.
Alisema kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Umoja wa Wanadiaspora waliorudi nchini waitwao Tanzania Diaspora Initiative (TDI).
“Kongamano hilo litasaidia wanadiaspora kuweza kuona fursa zilizopo nchini, kuvutia wawekezaji wageni kuwekeza Tanzania, kukuza utalii nchini, kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa diaspora pamoja na kuunganisha wawekezaji wa Tanzania na walioko nje ya nchi,” alisema waziri mkuu.
Mada kuu ya kongamano hilo ni “Connect, Engage, Inform and Invest” na kauli mbiu yake ni “Nyumbani ni Nyumbani”. Aliwataka wajitokeze kwa wingi kushiriki kongamano hilo alilosema limeandaliwa mahsusi kwa ajili yao na wasipojitokeza kwa wingi halitakuwa na maana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment