Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 16, 2014

Chadema yaibuka na mkakati mpya


Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.PICHA|MAKTABA 
Na Elias Msuya, MwananchiDar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeweka bayana mkakati wake mpya wa kushika dola kwa kukita mizizi yake tangu ngazi ya shina hadi ya Taifa.
Mkakati huo, ambao Chadema ilisema unalenga kukiondoa chama hicho kutoka kwenye uanaharakati na kukifanya kuwa chama cha dola, umekuja wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema chama hicho tayari kimeunda matawi 196,000 kati ya 250,000 yanayokusudiwa.
“Chadema imeshajiondoa kwenye harakati na kwenda kuwa chama dola. Tumefanya harakati kwa zaidi ya miaka 20 tukiwa na lengo la kukipeleka chama kwa wananchi, ili wakielewe na wakiheshimu, lakini sasa umefika wakati wa kujiandaa kushika dola,” alisema Dk Slaa.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Chadema ilishika nafasi ya pili kwa kuingiza wabunge wengi huku mgombea wake wa urais akishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete, ambaye ushindi wake ulipungua kutoka zaidi ya asilimia 80 hadi asilimia 61.
Mkakati wa chama
Dk Slaa alisema chama hicho kikuu cha upinzani kwa sasa kinafanya kazi katika kanda 10, nane zikiwa Bara na mbili Zanzibar na kanda hizo zimepewa mamlaka hadi ngazi ya chini (msingi).
“Baada ya kuunda kanda hizo 10 kumekuwa na mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na kuunda misingi au mashina. Leo tuna mabalozi wa nyumba 10 nchi nzima. Mwanachama wetu akipata shida, hana haja ya kwenda kusuluhishwa na balozi wa CCM,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Katika ngazi ya vitongoji tuna matawi au shehia kule Zanzibar. Lengo letu lilikuwa ni matawi 250,000 hadi sasa tuna matawi 196,000.”
Dk Slaa alisema kuwa chama hicho kiliahirisha uchaguzi mkuu mara tatu ili kukijenga kwanza katika ngazi za chini ikiwa pamoja na kufanya chaguzi katika ngazi hizo.
Akizungumzia uchaguzi wa ngazi ya majimbo, Dk Slaa alisema ulishaanza tangu Machi 26, mwaka huu na baadhi ya wilaya zimeshakamilisha.
Aliongeza kuwa baada ya uchaguzi wa majimbo, utafuata uchaguzi wa wilaya kuanzia Julai 18 hadi 22 utakaofuatiwa na rufaa kwa wasioridhika na matokeo.
Kwa habari ziaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Chadema-yaibuka-na-mkakati/-/1597296/2385604/-/qt61gdz/-/index.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment