Writen by
sadataley
6:34 PM
-
0
Comments
Mkutano wa kimataifa wa
maswala ya malipo ya uzeeni barani Afrika umeanza Jumatatu mjini Abuja
nchini Nigeria. Hii ni mara ya kwanza mkutano kama huo kufanyika Afrika.
Kwa sasa Nigeria ndiyo nchi iliyo na uchumi mkubwa Afrika na ina nafasi kubwa ya kukuwa.Lakini ukuwaji Afrika una athari kwa malipo ya uzeeni na masuala yanayoambatana na malipo hayo.
Dhamira ya mkutano huu ni mataifa kubadilishana ujuzi kati ya wataalamu wa malipo hayo kutoka Afrika na kushinikiza maendeleo katika masoko ya malipo ya uzeeni.
Malipo miongoni mwa nchi
Mkutano huo unafanyika ikiwa nchini Uganda miongoni mwa mataifa mengine Afrika, wafanyakazi waliostaafu inawachukua mda mrefu kuanza kulipwa malipo yao, na wengine wana fariki kabla ya kupata malipo yao.
Kwa upande mwingine Afrika kusini inafahamika kuwa nchi inayotoa malipo makubwa ya uzeeni katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara.
Na kwa hivyo huenda Afrika ina uwezo wa kubadilishana mipango kutoka kwa nchi nyengine zilizo na uchumi wa kukuwa.
Sehemu ya kwanza ya mkutano huu uliopewa jina 'Africa Special', utaangazia mafunzo makuu yanayotokana miongoni mwa mataifa Africa, uwekezaji, jinsi ya kukabiliana na hatari, sheria muhimu, teknolojia na mawasiliano.
Mkutano huu utafanyika Afrika kwa miaka mitano ijayo kutoka kikao hiki cha kwanza cha ufunguzi.
No comments
Post a Comment