Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Wednesday, June 25, 2014

Watanzania kunyongwa China


Dawa za kulevya aina ya Heroine
zaidi ya Watanzania 50 wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Idadi hiyo ni kati ya Watanzania 403 wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,uratibu na Bunge nchini humo,William Lukuvi ametaja baadhi ya nchi ambazo Watanzania wanashikiliwa kuwa Kenya,Uganda,Botswana,Malawi,Msumbiji, China,Brazil,Marekani,Pakistani na Uturuki.

Serikali ya Tanzania imekamilisha muswada wa sheria ya dawa za kulevya ambao ikiwa utapitishwa bungeni utasaidia harakati za kupambana na biashara ya dawa za kulevya.

kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia mwezi Januari mpaka juni mwaka huu,kiasi cha kilo 220 za dawa za kulevya aina ya Heroine na watuhumiwa 18 walikamatwa pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa sambamba na watuhumiwa saba.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment