Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 14, 2014

Wapenzi wa kandanda duniani waelekeza macho yao Brazil.

Wacheza carnival wakicheza samba huko  Sao Paulo, Brazil.
Wacheza carnival wakicheza samba huko Sao Paulo, Brazil.
Wapenzi wa kandanda duniani wanaelekeza macho yao brazil leo ambako fainali za kombe la duniani zinaanza kwa mechi kati ya wenyeji Brazil na Croatia – lakini wabashiri  wanatarajia kuwa Brazil itaibuka mshindi.
 Serikali imetumia dola billioni 11.5 kutayarisha mashindano haya yatakayo fanyika kwa mwezi mmoja kwa kujenga na  kuviboresha viwanja katika miji kumi na miwili ikishirikisha  timu 32 .

Waandamanaji wameandamana leo, wakiendelea kuikosoa serikali kwa jinsi ilivyotumia pesa vibaya badala ya kushughulikia mambo mengine muhimu. Mashindano haya yataanza kwa sherehe za ufunguzi  huko Sao Paulo kabla ya Brazil kupambana na Croatia.

Timu hii  wenyeji  inajaribu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita na mara ya kwanza tangu 2002. Timu zingine zinazopewa nafasi ya kushinda kombe hilo ni pamoja na Argentina, Spain, na Ujerumani ambayo kwanza lazima ishinde katika kundi liitwalo “kundi la kifo.’
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment