Writen by
sadataley
3:16 PM
-
0
Comments
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la
SAUT Kambarage ambapo aliwaambia kuwa wasomi wa vyuo wanatakiwa
kuchangia mawazo yao kwenye chama ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko
hasa ya kiuchumi ,alisema ni vyema kuja na mikakati ya kuonyesha uchumi
umepanda kwa mwananchi kuliko huu wa sasa ambao unaonyesha uchumi
umepanda lakini ni uchumi wa kwenye makaratasi.Uongozi Tawi la SAUT
Kambarage ulimualika Katibu wa Itikadi na Uenezi kuja kushuhudia
makabidhiano ya Uongozi na tathmini ya Tawi kwa miaka minane sasa.
Aliyekuwa Rais
wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha SAUT Mwanza Ndugu Dova Mcheshi
akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhiana Uongozi wa Tawi la SAUT
Kambarage ambapo aliwaambia wanachama wa CCM katika Chuo cha SAUT kuwa
kuanzia sasa chama kinajiimarisha zaidi kwenye Chuo cha SAUT.Dova
laiyekuwa CHADEMA lakini sasa amejiunga na CCM .Wadada wakiwa wamependeza na Sare yao ya Chama.
Viongozi wa CCM mkoani Mwanza na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.
Wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage,Mwanza.
No comments
Post a Comment