Writen by
sadataley
11 years ago
-
0
Comments
Huduma ya AFLEWO inakukaribisha katika Mkesha wa Kusifu,Kuabudu na
Maombi kwa ajili ya Afrika na Tanzania.Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka
Makanisa mbalimbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakimsifu
Mungu.Waumini,Wachungaji na Maaskofu watakusanyika kumwomba Mungu hasa
kwa mchakato mzima wa Katiba mpya na Uchaguzi mkuu 2015.
Mkesha huu maalumu,Utafanyika katika Kanisa la City Christian Center Upanga(CCC) karibu na Chuo cha Mzumbe,Siku ya Ijumaa 13/06/2014
Mchungaji Deo Lubala |
Chimbuko
Mchungaji Lubala anaeleza chimbuko la Aflewo kuanzia Chuo Kikuu cha
Daystar jijinii Nairobi, ambapo wanachuo walikuja na wazo la kumuimbia
Mungu, na hapo katika kuomba, mungu akawapa maono na hidima ikaitwa
Afrika tumuabudu Mungu, na wazo lilipofika Tanzania, ndipo kwa mara ya
kwanza tukio hilo likawepo mnamo mwaka 2011.
"kama ilivyo maono yenyewe halisi kwasababu lengo lake ni kumuabudu
Mungu, lazima tumtangulize Mungu, na kwa kuwa ni tukio la Kimungu,
lazima wenye matatizo yao yatatuliwe" anaeleza Mchungaji Lubala ambaye
ni mmojawapo wa walezi wa tukio hili ambalo halina kiingilio.
Tukio hili ambalo limekuwa likifanyika baraka kila linapokuwepo,
limepata baraka kutoka kwa wachungaji mbalimbali, hasahasa ikizingatiwa
kuwa ibada ya kuabudu ni jambo ambalo linamsogeza mtu karibu zaidi na
Mungu, na ku'experience' mguso wa kipekee.
Milango siku hiyo itakuwa wazi mapema, ambapo watu wanashauriwa angalau
kufika saa kumi na mbili ili kujipatia nafasi nzuri, na kisha ibada
kuanza saa moja jioni.
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu namba +255712207717.
Tukutane Upanga, City Christian Church kesho Ijumaa...
Tukutane Upanga, City Christian Church kesho Ijumaa...
Habari na Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment