Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Thursday, June 12, 2014

Soko la Karume Dar es Salaam lateketea


Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa la mitumba la karume huko Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.
Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha kutengeneza bia cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kufuatana na mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.

Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment