Writen by
sadataley
3:04 PM
-
0
Comments
Na Fidelis Butahe na Sharon Sauwa, MwananchiDodoma. Kitendo cha Mahakama kufungua milango
kwa mawaziri na wabunge kufunguliwa mashtaka kutokana na kauli
watakazozitoa bungeni ambazo ni kinyume cha Katiba na Sheria,
kimeonekana kuwachanganya viongozi hao ambao wamesema kuwa wanalindwa na
sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.
Wamesema licha ya kuwa kazi ya Mahakama ni
kutafsiri sheria, Bunge kutunga na Serikali kusimamia sheria, nchi
nyingi duniani wabunge wake wana kinga na hawashtakiwi kwa kauli
watakazozitoa bungeni.
Kauli za wabunge hao zimekuja ikiwa imepita siku
moja tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kutoa msimamo huo wakati
ikitoa uamuzi wa pingamizi la awali katika kesi ya kikatiba iliyokuwa
ikimkabili Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililowasilishwa na Jopo la
Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(DAG, George Masaju.
Kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013 ilifunguliwa na
Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana
na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), dhidi ya Pinda na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG), aliyeunganishwa kama mlalamikiwa wa pili.
Mahakama Kuu katika uamuzi wake juzi ilikubaliana
na baadhi ya hoja za mawakili wa utetezi (Serikali) na kuitupilia mbali
kesi hiyo, lakini ikatamka kuwa wabunge na mawaziri wanaweza kushtakiwa
kwa kauli au jambo walilolitamka bungeni, linalokiuka sheria na haki za
binadamu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili,
Naibu Spika Job Ndugai alisema, “Mahakama ikisema, imesema licha ya kuwa
Katiba inaeleza wazi kuwa Bunge lipo huru.”
Alisema kuwa suala hilo linaweza kuwekwa sawa katika Katiba Mpya ambayo mjadala wake utaendelea Agosti mwaka huu.
“Nchi nyingi duniani wabunge wana kinga kwa kauli
zao watakazozitoa bungeni. Kama hapa kwetu tumeamua hivyo ni sawa tu,
ila mashtaka yatakuwa mengi kwelikweli,” alisema Ndugai.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla (CCM)
alisema, “Sidhani kama tafsiri hii ni sahihi sana kwa sababu wabunge
wanalindwa na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.”
Kigwangalla alisema sheria hiyo ipo wazi kwamba
mbunge akizungumza lugha isiyofaa mtu ambaye anataka kuchukulia hatua
anatakiwa kuiandika barua Ofisi ya Bunge.
“Barua hiyo itakwenda kwa Spika wa Bunge na kama
akiridhika atalipeleka suala hilo katika Kamati ya Kinga, Haki na
Madaraka ya Bunge ambayo inaweza kumwita mlalamikaji ili kumsikiliza,”
alisema Kigwangalla.
Alifafanua kuwa sheria hiyo haijawahi kufanyiwa
marekebisho na kama mahakama imetoa tafsiri hiyo maana yake ni kwamba
kesi za wabunge zitarundikana mahakamani.Kwa habari kwa kina ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mvutano-mkali-Bunge--Mahakama/-/1597296/2341018/-/15o9be5/-/index.html
No comments
Post a Comment