Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 17, 2014

Mashambulizi ya pili Mpeketoni, Kenya


Picha za kusikitisha za watu waliouawa na kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa Mpeketono Jumapili usiku
Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment