Writen by
sadataley
11:35 AM
-
0
Comments
Na Fidelis Butahe na Edwin Mjwahuzi, MwananchiDodoma. Makamu mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Philip Mangula amesema kituo hicho kimekumbwa na mpasuko baada ya vyama vya Chadema na CUF kususia kikao kilichoitishwa Jumapili iliyopita.
Kitendo cha vyama hivyo kutoonekana kumetafsiriwa
kama mwendelezo wa kile kilichotokea katika Bunge Maalumu la Katiba
Aprili 16, baada ya wapinzani kususia vikao kutokana na kutokuridhishwa
na mwenendo wa chombo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika
ofisi za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini hapa, Mangula
ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa CCM, alisema kikao hicho kililenga
kujadili mwenendo wa vyama na athari zake kisiasa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema
viongozi wa vyama vya siasa huitwa kwa mialiko. “Sikuona ulazima wa
Mangula kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza jambo hili,”
alisema. Mbowe alisema Chadema na CUF si wanachama pekee wa TCD.
No comments
Post a Comment