Writen by
sadataley
6:25 PM
-
0
Comments
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dodoma. Macho na masikio ya wananchi leo yatahamia bungeni mjini Dodoma wakati Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum atakapokuwa akisoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Mwelekeo wa Bajeti hiyo umekuwa na usiri mkubwa
kutokana na Serikali kutokuwa wazi kuieleza Kamati ya Bunge ya Bajeti,
vyanzo vyake vipya vya mapato licha ya kukutana mfululizo tangu Juni 5,
mwaka huu.
Licha ya wabunge kutaka kufahamu Serikali
itazipataje Sh19 trilioni kugharimia Bajeti ya 2014/15, wakati
imeshindwa kutimiza malengo ya kukusanya Sh18.2 trilioni kwa mwaka huu
wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu, vyanzo hivyo vimekuwa siri
kubwa. Bajeti ya mwaka huu wa fedha ina upungufu wa Sh1.8 trilioni.
Hata hivyo, habari kutoka katika kikao hicho
zinaeleza kuwa usiri huo unatokana na Serikali kutokuwa na vyanzo vya
uhakika vya mapato, jambo ambalo limewafanya kutotaka kuliweka wazi.
“Hakutakuwa na jipya katika upande wa vyanzo vipya
vya mapato, tutarajie vyanzo vilevile vya Bajeti ya mwaka 2013/14
ambavyo vilitokana na kuongeza kodi katika vinywaji baridi; soda, bia na
maji, pia katika sigara,” kilisema chanzo hicho.
Kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato
kumekwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika wizara zote
kwani Bajeti ya mwaka 2013/14 imetekelezwa kati ya asilimia 25 hadi
35.Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hivi karibuni kuwa
wizara yake inakusudia kupitia upya bajeti za wizara zote ili kuhamisha
fedha kutoka katika matumizi yasiyo ya lazima ili zielekezwe katika
mahitaji muhimu.
Katika kuthibitisha hilo, Kamati ya Bajeti na
Serikali zilikubaliana kukata asilimia 7.5 ya fedha katika baadhi ya
mafungu ya matumizi mengineyo (OC) kutoka katika wizara zote ili
kuwezesha kupatikana kwa Sh230 bilioni ambazo zinahitajika kwa ajili ya
maendeleo, hasa katika sekta tatu; afya, miundombinu na kilimo.
“Tunajibana ili fedha zipelekwe katika maji,
elimu, miundombinu na afya. Zitakazobaki zitapelekwa katika maeneo
mengine,” alisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na
Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.
Katika Bajeti ya mwaka 2014/15, huenda Serikali
ikaja na tozo mpya ili kupata fedha za kuanzisha mfuko wa maji kutokana
na kelele zilizopigwa na wabunge, kwa maelezo kuwa ni idadi ndogo ya
Watanzania wanaopata maji salama.
Jambo jingine linalosubiriwa kwa hamu ni ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani (Mei Mosi), ya kupandisha mishahara ya wafanyakazi.
Pia Rais aligusia kupunguzwa kwa Kodi ya Mapato ya
Wafanyakazi (Paye) na kuahidi kuipunguza kutoka asilimia 13 ya sasa na
kufikia tarakimu moja.
Wafanyabiashara wakubwa nao wanaisubiri Bajeti
hiyo kujua kama watapata unafuu wa kodi ya mapato, huku wafanyabiashara
wadogo wakitaraji kuondolewa kodi.
Kwa habari zaidi ighttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kitendawili-cha-Bajeti-kuteguliwa-leo/-/1597296/2345250/-/ngndomz/-/index.htmlia
Kwa habari zaidi ighttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kitendawili-cha-Bajeti-kuteguliwa-leo/-/1597296/2345250/-/ngndomz/-/index.htmlia
No comments
Post a Comment