Writen by
sadataley
11:21 AM
-
0
Comments
Wahenga walisema, kila zama na kitabu chake, ndivyo ilivyo siyo
tu kwa watawala, bali hata maisha ya kila mwanadamu yana ‘kitabu chake.’
Hilo linaweza kuthibitishwa na mambo mbalimbali,
lakini kwa namna ya pekee historia ya Mwanasheria, aliyekuwa pia Mbunge,
Naibu Waziri na sasa mkulima, Jaji Mstaafu Edward Mwesumo.
Katika mahojiano na Mwananchi Jumamosi, Jaji
Mwesumo ambaye sasa anaishi eneo la Sagamaganga, Ifakara katika Wilaya
ya Kilombero mkoani Morogoro anaeleza mengi yaliyomkumba wakati wa zama
zake za utumishi, akiwa amebahatika kuhudumu mihimili mitatu ya dola
ambayo ni Mahakama, Bunge na Serikali.
Alianza utumishi mwaka 1962 katika iliyokuwa Wizara ya Ardhi, Maliasili na Wanyama wakati huo akiwa karani.
Anasema baada ya miezi minne kazini, alijiunga na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 1965 alihitimu Shahada ya Sheria.
Mwaka 1966 aliajiriwa na Serikali na kufanya kazi ya uhakimu katika
mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Singida, Tanga na Dodoma hadi mwaka
1971.
“Nilifanya kazi katika idara ya Mahakama kwa ngazi
tofauti hadi kuwa Jaji wa Mahakama tangu mwaka 1966 hadi mwaka 1980,”
anasimulia Jaji Mwesumo.
Kesi anayokumbuka
Akizungumzia utendaji wake katika idara ya
Mahakama iliyo na kazi ya kutafsiri sheria, Jaji Mwesumo anasema
anakumbuka mambo mengi mazuri, lakini moja kubwa ni kesi ambayo mwishowe
ilisababisha yeye kuondoka kwenye nafasi ya ujaji aliyokuwa nayo.
Anasimulia kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 1979
aliposimamia kesi ya kwanza ya kikatiba nchini katika Mahakama Kuu
mkoani Arusha.
“Nakumbuka wakati huo Rais wa Zanzibar na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Aboud Jumbe aliwaweka watu kizuizini.
Wakati huo mimi kituo changu cha kazi kilikuwa Arusha na bosi wangu
alikuwa Jaji Nassoro Mnzava.
“Happy Makole na Wamasai watatu waliwekwa kizuizini kwa amri ya Rais Jumbe ambaye alisema kuwa watu hao ni hatari kwa nchi.
“Watu hao waliweka mawakili watatu, walikuwa ni
James Mwale na wenzake ambao walifungua kesi kupinga amri hiyo ya Rais.
Bosi wangu, Mnzava akanipangia kesi hiyo, niliisikiliza kwa hatua mbili.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Jaji-Mwesumo--Aboud-Jumbe-alisababisha-niache-kazi/-/1597296/2348056/-/5e8wwq/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Jaji-Mwesumo--Aboud-Jumbe-alisababisha-niache-kazi/-/1597296/2348056/-/5e8wwq/-/index.html
No comments
Post a Comment