Writen by
sadataley
10:59 AM
-
0
Comments
Akizungumza kwa uchungu baada ya kusikia taarifa
ya kuzorota kwa afya ya mtoto Eliud, daktari Bokhary ambaye yupo
masomoni nchini Misri alisema: “Usinilize jamani naona uchungu, naomba
tushauriane nini cha kufanya...yaani hadi tumbo linaniuma.
“Roho inaniuma sana kusikia utumbo wa Eliud uko
nje, ingekuwa siyo shule ningekaa nao hadi wapone kabisa,” alisema
Bokhary, ambaye alisisitiza kwenda Mbeya kuwaona watoto hao.
Afya ya Eliud yazorota
Hali ya mtoto Eliud inazidi kuwa mbaya kutokana na
sehemu kubwa ya utumbo wake mpana unaotumika kutolea haja kubwa kutoka
nje hali inayomfanya kudhoofu kiafya.
Baba mzazi wa watoto hao, mkazi wa Kasumulu Kyela,
Eric Mwakyusa alisema jana kuwa hali ya mtoto wake inazidi kumchanganya
kutokana na kuzidi kubadilika kila wakati.
Hivi karibuni alisema baada ya hali ya mtoto huyo
kubadilika alimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Kyela ambako daktari
aliyemwona alishauri mtoto huyo asubiri hadi atakapokwenda India, Agosti
mwaka huu. Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Festo Dugange
aliliambia gazeti hili kuwa hajawahi kusikia wala kumwona mtoto
aliyetoka utumbo hospitalini hapo.
Wakati huohuo, baba wa watoto hao, Mwakyusa amepewa msaada wa pikipiki na msamaria mwema ili kukidhi maisha yake.
Mwakyusa amewashukuru wasamaria mbalimbali
wanaomsaidia kwa njia tofauti ikiwemo wasamaria waliompatia pikipiki ili
afanye kazi ya kubeba abiria na mapato yake yatumike kuboresha maisha
ya familia yake.
‘’Nawashukuru waandishi wa Mwananchi kwa kuandika
hali halisi ya watoto wangu, kwani jana nimepewa pikipiki na msamaria
mwema wa jijini Dar es Salaam ambaye alipata taarifa za watoto wangu
kupitia magazeti yenu’’, alisema.
Alisema kwa kipindi kirefu alikuwa akiendesha
pikipiki ya mtu ambaye alikuwa akipewa Sh8,000 kila siku na yeye kubaki
na kati ya Sh1,000 au 2,000 kwa siku ambazo ndizo zilikuwa zikitumika
kuwahudumia watoto na familia nzima.
No comments
Post a Comment