Writen by
sadataley
2:49 PM
-
0
Comments
Kiongozi mmoja wa kanisa la kianglikana anayehusika
katika majadiliano ya kuwaachilia huru mamia ya wasichana waliotekwa
nyara nchini Nigeria amesema kuwa wengi wao wanazuiliwa nje ya taifa
hilo katika kambi tatu tofauti.
Daktari Steven Davis ambaye ni raia wa Australia
ameiambia BBC kwamba wenzake waliwaona baadhi ya wasichana hao ambao
walikuwa wakioga na upande mwengine kuwapikia waliowateka kutoka kwa
kundi la wanamgmbo wa Boko Haram.Davis amesema kuwa majadiliano ya kutaka kuwachiliwa kwa wasichana hao karibia yafue dafu kabla ya baadhi ya makamanda wa kundi hilo kulipinga wazo hilo dakika za mwisho wakihofia kukamatwa.
Amesema juhudi zozote za kuwanusuru wasichana hao kwa nguvu hazitafua dafu.
No comments
Post a Comment