Writen by
sadataley
6:31 PM
-
0
Comments
Viongozi wa mashitaka nchini
Brazil , wanachunguza madai kuwa viungo vya miili vinatolewa kwa miili
ya watu wasiojulikana na kuuzwa kwa ajili ya utafiti wa kimatibabu.
Viongozi wa mashitaka wameambia BBC kuwa viungo
vinataolewa kwa miili ya watu waliofariki bila ya kufanyika juhudi za
kuwatafuta jamaa zao watu hao ili kupata ruhusua kutoka kwao.Hadi hivi karibuni, maiti zilizopatikana kando ya barabara au katika hospitali za umma huzikwa katika makaburi ya umma ikiwa hakuna aliyekuja kudai miili hiyo kwa muda wa masaa 72.
Hata hivyo moja ya shirika linalodaiwa kufanya uhalifu huo wa kuuza viungo vya miili ya watu wasiojulikana limekanusha madai hayo.
Uchunguzi huu ulioanza mjini Sao Paulo, mwaka jana, ulianzishwa na polisi kutokana na madai ya familia kwamba maafisa wakuu hawakuwashauri kabla ya kuzika jamaa zao waliofariki katika makaburi ya umma ya Perus.
Baadaye mmoja wa walioshuhudia vitendo hivyo walifahamisha polisi kuwa viungo hutolewa kwa miili ya wafu na kutumiwa kwa utafiti wa kimatibabu bila idhini ya jamaa wa wafu.
Hata hivyo viongozi wa mashitaka wanasema kuwa hawana ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai ya biashara ya viungo vya binadamu.
Shirika la SVO linaloendeshwa na walimu kutoka katika chuo kikuu cha Sao Paulo, linasema kuwa kwa kawaida wao hutumia miili tu ambayo imeshatambulishwa wanapotafuta viungo vya utafiti.
Walimu hao wanasema huwa hawatumii miili ambayo wenyewe hawajulikani.
No comments
Post a Comment