Writen by
sadataley
4:36 PM
-
0
Comments
Upendo Nkone |
Mida ya mchana wakati tamasha ndo linaanza anza, watu bado ni kama
walikuwa hawajielewi, lakini kadi mambo yalivyokuwa yakisonga, ndivyo
hali ikabadilika pia, ambapo Faraja Ntaboba, muimbaji kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo aliwagusa watu kwa acapella ya 'mtu mwembamba',
ambapo walikuwa wakishangilia kwa sana, na kisha baadae alipoanza kuimba
ndani ya mavazi yake nadhifu, wala hakujali vumbi la uwanja wa
Kambarage, ila alienda nayo hadi chini akabilingita, huyo aliwamaliza
watu.
Upendo wote wawili walikuwepo, na pale alipoanza kuimba mama Askofu
Upendo Nkone, hapo ndipo nikakumbuka kuwa jukwaani kuna watu - watu
walio hai, kwani kwa kuwagusia tu 'usifurahi juu yangu, ee adui
yaaaanguuuu', watu wote uwanjani nao haoo 'niangukapo miiiimi,
nitasimama teeena'. Na kisha baadae akaimba nyimbo mbili, Niacheni
Niimbe, na Upendo wa Yesu. Watu walikuwa live kutoka kwenye siti zao.
Alipomaliza kuimba, siyo kwamba ndio alimaliza kuhudumu, kwani maombi
yafakata kama kawa, na kuna ambao waliona ya kwamba hayatoshi, wakaamusa
kumuendea hukohuko aliko, nao wakaachiliwa uponyaji kwa jina la Yesu.
Upendo Kilahiro, Mess Jacob Chengula, Tumaini Njole, Grace Mwikabwe, The
Voice (watoto wa nyumbani), Caana Choir FPCT, na KKKT Usharika wa
Ebeneza Shinyanga Mjini ni baadhi tu ya waimbaji ambao walikuwepo
kumrudishia sifa na utukufu BWANA Yesu.
Hebu tazama picha za matukio kama ambavyo Gospel Kitaa ilikuwepo ili kuyanasa na kukufikishia bila wasiwasi.
MAMA ASKOFU UPENDO NKONE
Maaombi nii muhiimuuuu |
MASHUHUDA WAKIENDA SAWA
HABARI NA PICTURE KWA HISANI YA Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment