Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, May 3, 2014

Vita vya ndugu kupiganiwa ugenini

 
 Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia baada ya kuitoa Bayern Munich nusu fainali Uefa
Timu tatu za Hispania zimefanikiwa kucheza fainali mbili tofauti za mashindano yenye hadhi ya juu barani Ulaya mwaka 2014.
Timu hizo mahasimu zimefikia hatua hiyo baada ya Real Madrid kuwachabanga waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya mabao 5-0. Real Madrid ilipata ushindi wa bao 1-0 nyumbani, huku ugenini ikiisambaratisha Bayern magoli 4-0.




Nayo Atletico Madrid baada ya kushindwa kuifunga Chelsea katika uwanja wa nyumbani kwa kutoka suluhu ya 0-0, katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali katika uwanja wa Stanford Bridge jijini London, Chelsea ilikiona cha moto kwa kuchabangwa magoli 3-1.

Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia moja ya magoli yao
Hivyo vita vya ndugu hao Real Madrid na Atletico Madrid vitapiganiwa ugenini katika uwanja wa Estádio do Sport Lisboa e Benfica, ujulikanao pia kama Estádio da Luz (uwanja wa mwangaza)mjini Lisbon, Ureno, Jumamosi tarehe 24 Mei 2014.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967, fainali za kombe la ligi ya mabingwa la UEFA zinafanyika mjini Lisbon.
Baadhi ya wachezaji wa Sevilla walioitoa Valencia
Katika fainali nyingi za kombe la ligi ya Europa, Sevilla ya Hispania inapambana na Benfica ya Ureno mchezo utakaopigwa katika dimba la Turin, nchini Italia Jumatano tarehe 14 Mei 2014.
Sevilla imefuzu kucheza fainali hizo baada ya kuwatoa ndugu zao Valencia katika mchezo wa nusu fainali baada ya matokeo ya 3-3 lakini ikinufaika na goli la ugenini. Katika mchezo wa awali wa nusu fainali, Sevilla iliibuka na ushindi wa 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani, lakini ikapata kipigo cha 3-1 ugenini na kufanya matokeo kuwa 3-3.
Kwa upande wake Benfica katika mchezo wa kwanza iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Juventus ya Italia na ugenini ikatoka sare ya kutofungana na wenyeji Juve, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment