Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, May 22, 2014

Urusi yaudhiwa na kauli ya Prince Charles

Naibu balozi wa Urusi mjini London ameomba kukutana na maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa Uingereza kujadili matamshi ya Mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles ambapo amefananisha vitendo vya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Ukraine na uliokuwa utawala wa kinazi nchini Ujerumani chini ya Adolf Hitler.
Prince Charles ambaye yuko kwenye foleni kumrithi Malkia wa Uingereza , alitoa matamshi yake Jumatano alipokuwa anazungumza na mfanyakazi mmoja wa Poland katika makavazi ya wahamiaji eneo la Nova Scotia.
Walikuwa wanajadili hatua ya Hitler kunyakua nchi wakati wa utawala wake wakati ambapo mwanamfalme huyo alipofananisha kitendo hicho na kilichofanyika nchini Ukraine kwa maagizo ya Rais Vladimnir Puti.
Prince Charles anatarajiwa kuhudhuria hafla moja nchini Ufaransa mwaka ujao.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, amesema kuwa sio jambo la kawaida mwanamfalme kutoa kauli za kisiasa wakati wa mzungumzo ya faragha na kwamba kwa sasa hawawezi kutamka lolote kuhusu zogo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu, Prince Charles na mkewe Camilla walitembelea makavazi ya kitaifa ya wahamiaji nchini Canada, wakati wa ziara yao ya siku nne nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema kuwa ombi la kufanyika mkutano ni dalili ya Urusi kukasirishwa na matamshi ya Prince Charles ingawa Urusi imejizuia kugeuza swala hilo na kulifanya kuwa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
Inaaminika kuwa Urusi inataka ufafanuzi kuhusu matamshi ya Mwanamfalme huyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment