Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 21, 2014

Urusi na Uchina zasaini mkataba wa gesi

Rais Vradimir Putin(kushoto) na Rais Xi Jinping(kulia)
 Rais wa Urusi Vradimir Putin akisalimiana na mwenzake wa Uchina Xi Jinping
Urusi imekubali kuipatia Uchina gesi , kufuatia mkataba wa mabilioni ya dola ambao mataifa hayo mawili yamekuwa yakiujadili kwa kipindi cha muongo mmoja .
Mkataba huo unadhaniwa kuwa wenye thamani ya dola bilioni mia nne na utadumu kwa zaidi ya miaka thelathini.
Wachambuzi wanasema kuwa matatizo ya kisiasa ya Urusi na mataifa ya magharibi kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine, yameisukuma Urusi kukamilisha mkataba huo na Uchina, ili kupata soko la rasilimali yake.
Mapatano hayo yamesainiwa katika sherehe zilizofanyika mjini Shanghai na kuhudhuriwa na rais wa Uchina , Xi Jinping, na mwenzake wa Urusi , Vladimir Putin.
Source  http://www.bbc.co.uk/swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment