Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 6, 2014

Seif, Lipumba waongoza waombolezaji mazishi ya Sheikh Ilunga Dar es Salaam


Waumini wa dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa Sheikh Hassan Ilunga kabla ya kumzika katika Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es Salaam, jana. Picha na Joseph Zablon 
Na Joseph Zablon, Mwananchi
Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad jana alikuwa miongoni mwa maelfu ya waumini wa Kiislamu waliojitokeza kumzika Sheikh Hassan Ilunga aliyefariki dunia Dar es Salaam juzi kwa maradhi ya kupooza.
Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF aliongozana na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba katika ibada ya kuaga mwili wa sheikh huyo, kabla ya maziko yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa.
Akizungumza kabla ya ibada ya maziko, Amiri wa Shura ya Maimamu, Sheikh Mussa Kundecha alisema marehemu alipata matibabu ya figo huko India na Aprili mwaka huu alirejea nyumbani.
“Akiwa huko (India), alianza kutokewa na matatizo mapya ikiwa ni pamoja na baadhi ya viungo vyake kupooza au sijui tuseme kufa ganzi na mara ikawa leo mguu kesho unarudi hali ya kawaida na hali hiyo ikawa inajirudiarudia,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Sheikh Kundecha alisema madaktari hawakubaini ugonjwa uliokuwa unamsumbua ndipo alipopewa ruhusa ya kurudi nchini.
“Aliporudi alikuwa anazungumza vizuri na kuwasiliana bila shida na watu wengine, ingawa kuanzia katika kiuno kwenda chini viungo havikuwa na mawasiliano mazuri na mwili,” alisema na kuongeza kuwa siku tatu kabla ya mauti alipoteza fahamu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment