Writen by 
                            sadataley
3:56 PM
                            - 
                            
0
                            Comments
                          
Yerusalemu, Israel. Malumbano makali ya maneno 
na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa 
Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani 
aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.
Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya 
siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni 
ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika 
ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati 
akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.
Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo.
Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”
“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.
Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia 
tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya 
Papa Francis katika nchi takatifu.
Mtaalamu wa masuala ya lugha, raia wa Israel, 
Profesa Ghil’ad Zuckermann ameliambia Shirika la Habari la Reuters 
kwamba wawili hao, Netanyahu, ambaye ni mtoto wa mtaalamu wa historia ya
 Kiyahudi na Papa Francis, kiongozi wa kiroho anayeongoza waumini 
bilioni 1.2 Wakatoliki, kila mmoja ana hoja. “Yesu alikuwa mzungumzaji 
wa Kiaramaiki,” anasema Profesa Zuckerman kuhusu lugha hiyo ambayo 
imetoweka yenye uhusiano na Kiebrania. “Pia, anaweza kuwa alizungumza na
 kufahamu Kiebrania, lugha ambayo ilitumika kwenye maandiko.”
Prof Zuckermann alisema kuwa wakati wa Yesu, 
Kiebrania kilizungumzwa na watu wa madaraja ya chini - “ambao ndiyo 
aliowahubiria”. Mojawapo ya vitu vingi katika eneo la Mashariki ya Kati 
hadi sasa ni kuhusu utata wa Yesu, utata huo umechukua pia sura na 
mtazamo wa kisiasa.
Yesu, Myahudi alizaliwa kwenye mji wa Bethlehemu 
ambao ulikuwa chini ya himaya ya Warumi, kwenye Mkoa wa Yudea, katika 
ardhi inayoshikiliwa kwa sasa na Israel kwenye Ukanda wa Magharibi.
Alikulia mjini Nazareth , akaendesha utume kwenye 
mji mwingine wa Galilea, ambao pia uko kaskazini mwa Israel, alifia 
mjini Yerusalemu, mji ambao unatukuzwa na Wayahudi, Wakristo na 
Waislamu, ambao unagombewa na tawala za Israel na Palestina hadi sasa.
Kwa upande wao, Wapalestina wamekuwa wakidai kuwa 
Yesu ni Mpalestina. Hata hivyo, utawala wa Israel umekuwa ukipingana na 
mtazamo huo.
 
 
 
 
 
 
 
No comments
Post a Comment