Writen by
sadataley
1:30 PM
-
0
Comments
Dodoma. Serikali imetakiwa kutoa maelezo
bungeni, kuhusu sababu za kuuawa kwa waasisi sita wa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar wanaodaiwa kuzikwa katika handaki moja Zanzibar.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano), msemaji wake, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza
waasisi hao walifanya makosa gani.
Aliwataja waasisi hao kuwa ni Abdallah Kassim
Hanga aliyekuwa Waziri Mkuu, Abdulaziz Twala aliyekuwa Waziri wa Fedha
na Saleh Akida aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na viongozi
waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi, Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha
Ubwa ambao alisema waliuawa na kuzikwa handaki moja eneo la Kama,
Zanzibar.
Lissu alisema hayo huku akinukuu kitabu cha
‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’ kilichoandikwa na Harith Ghassany
alichosema kilionyesha jinsi viongozi hao walivyouawa na kuzikwa katika
kaburi moja.
“Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli
juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na
kuzikwa katika kaburi au handaki moja,” alisema Lissu huku wabunge
wakiwa kimya kumsikiliza.
Mgawo wa Zanzibar
Lissu pia aliibua mambo mazito kuhusu mgawanyo wa
fedha za misaada na mikopo ya kibajeti kati ya Serikali ya Muungano na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema Muungano ni kielelezo cha unyonyaji na ukandamizaji ambao nchi kubwa imeifanyia nchi ndogo ya Zanzibar kwa miaka mingi.
Alikwenda mbali na kuitaka Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar au Wazanzibari kwa umoja wao, kufungua kesi Mahakama za
kimataifa kudai fedha zote ambazo nchi yao imeibiwa kwa kivuli cha
Muungano.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, alisema hadi Machi mwaka huu, Zanzibar ilikuwa imepata gawio la
Sh27.1 bilioni badala ya Sh32.6 bilioni zilizoidhinishwa na Bunge, sawa
na asilimia 83.
Hata hivyo, alisema hilo linaweza lisiwe tatizo,
kwani kwa mwelekeo wa takwimu hizo, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa
fedha, gawio lililoidhinishwa linaweza kuwa limelipwa lote.
Haya hivyo, alisema tatizo kubwa na la msingi ni
kwamba, gawio lililoidhinishwa na Bunge si halali kwa Zanzibar, kwa
mujibu wa hotuba ya Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ya Aprili 30, mwaka
huu.
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz
No comments
Post a Comment