Writen by
sadataley
3:23 PM
-
0
Comments
Waziri mkuu mteule nchini India Narendra Modi
Kuna mwamko mpya wa kisiasa nchini India ambapo chama cha upinzani cha Hindu ,BJP kimeshinda uchaguzi uliokuwa na maamuzi makali kuwahi kufanyika nchini humo kwa kipindi cha miongo mitatu.
Wakati huohuo rais Barrack Obama wa Marekani amemkaribisha mjini Washington waziri mkuu mteule wa India Narendra Modi kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake.
Baadhi ya waliompigia kura waziri mkuu mpya Narendra Modi
Kabla ya uchaguzi huo,Marekani ilikuwa imekataa kumpa viza ya kuingia nchini humo bwana Narendra Modi kufuatia ghasia dhidi ya waislamu katika jimbo analotoka la Gujarati mnamo mwaka 2002.
lakini wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imesema kuwa kiongozi huyo hatakabiliwa na vikwazo vyovyote kwa kuwa kama kiongozi wa serikali atapewa viza maalum.
Baadhi ya viongozi waliompigia simu ili kumpongeza waziri huyo mteule ni waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron,waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif pamoja na mawaziri wakuu kutoka Israel na Australia.
No comments
Post a Comment