Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 23, 2014

Baraza la usalama laweka vikwazo dhidi ya kundi la Boko Haram.

Mshukiwa wa kundi la Boko Haram, Ali Sanda Umar Kondugaakiwa mahakamani akiwa na seneta  Ali Ndume  wakati wa kesi yake huko Nigeria November 22, 2011.
Mshukiwa wa kundi la Boko Haram, Ali Sanda Umar Kondugaakiwa mahakamani akiwa na seneta Ali Ndume wakati wa kesi yake huko Nigeria November 22, 2011.
Baraza la usalama la umoja mataifa limeweka vikwazo dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Nigeria Boko Haram, ambalo limefanya  wimbi la mashambulizi ya mauaji  na hivi karibuni kuteka nyara takriban wasichana mia tatu huko Nigeria.

Nigeria imeliomba baraza hilo kuongeza kundi hilo la wanamgambo katika orodha ya makundi yenye ushirikiano na al qaida, ambayo yamekewa adhabu ya  kuzuiwa kwa  mali zao,  vikwazo vya usafiri na marufuku ya  silaha.

Balozi wa Marekani kwenye  umoja Mataifa Bi.Samantha Power, alikaribisha hatua hiyo ya baraza, akiita hatua muhimu katika kuunga mkono  juhudi za serikali ya Nigeria kulishinda kundi la Boko Haram na kuwawajibisha viongozi wanaofanya mauaji kwa  ukatili waliotenda.

Nchini Nigeria, washambuliaji  waliokuwa na silaha waliwauwa takriban watu 29 jumatano jioni  katika shambulizi kwenye  kijiji cha mbali  upande wa  Kaskazini mashariki. Hilo lilikuwa shambulizi la tatu kubwa linalolaumiwa kufanywa na Boko Haram wiki hii.

Siku ya alhamisi, walimu kote nchini Nigeria  waliingia mitaani kwa maandamano ya siku moja kupinga utekaji nyara wa wasichana wa shule uliofanywa na Boko Haram. Wasichana hao wamepotea kwa zaidi ya mwezi sasa, na nchi kadhaa zimeahidi kuisadia Nigeria katika juhudi zake za kuwatafuta wasichana hao. 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment