Writen by
sadataley
1:11 PM
-
0
Comments
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana usiku
alikuwa katika wakati mgumu wakati Bunge lilipoketi kama Kamati ya
Matumizi, kiasi cha kutishia bajeti ya wizara yake kukwama.
Hata hivyo, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 yalipitishwa.
Wabunge wa vyama vyote walimbana Dk Mwakyembe na
kutoa shilingi karibu katika kila kifungu wakihoji mambo mbalimbali hasa
juu ya mgogoro wa umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda),
uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), usafiri wa majini
hususan usalama wa meli ya Mv Victoria.
Sakata la Uda
Sakata hilo la Uda lilisababisha mvutano baina ya
Naibu Spika, Job Ndugai na Dk Mwakyembe ambaye alilalamikia mjadala wa
Uda kuruhusiwa katika hotuba ya wizara yake.
Hata hivyo, Ndugai alipangua hoja hiyo akisema
mbali na kwamba Uda inagusa wizara nyingi, lakini ni suala linalohusu
uchukuzi hivyo ilikuwa sahihi kujadiliwa katika mjadala huo.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla ndiye
aliyeibua suala hilo kwa kuhoji sababu ya Serikali kutoa taarifa
zinazokanganya kuhusu Uda, hali kamati anayoiongoza ilishakaa na pande
zote husika wakiwamo wataalamu na kuwa na hitimisho kwamba Kampuni ya
Simon Group Ltd ni waendeshaji halali wa shirika hilo.
Hoja hiyo iliibua mjadala ambao pia ulichangiwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye alisema
Simon Group Ltd waliuziwa kihalali hisa za Uda na kwamba wamiliki hao
wanazongwa kutokana na kwamba ni ngozi nyeusi (Watanzania).
Kwa upande wake, Waziri Kivuli wa Uchukuzi, Moses
Machali alisema maelezo ya Serikali kuhusu umiliki wa Uda yana
mkanganyiko, hivyo Simon Group Ltd wanaandamwa bila sababu za msingi.
Kwa upande wake Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe alisema Serikali inajiweka uchi, kutokana na majibu
yanayokinzana kutoka kwa mawaziri na Kamati za Bunge.
Hoja ya Mbowe ilipingwa na waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), aliyesema Serikali haijajivua
nguo na kwamba itachukua hatua za kuliweka sawa kwa kutoa taarifa moja.
Awali, akihitimisha hotuba yake huku akipangua
hoja mbalimbali za wabunge, Dk Mwakyembe alisema mwaka 2012/2013 ilikuwa
ni kuitoa Sekta ya Uchukuzi kutoka katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Bajeti-ya-Mwakyembe-yatikisa-Bunge--yapita/-/1597296/2327686/-/g4x6iyz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Bajeti-ya-Mwakyembe-yatikisa-Bunge--yapita/-/1597296/2327686/-/g4x6iyz/-/index.html
No comments
Post a Comment