|
Mheshimiwa Samuel Sitta akiwahsukuru wajumbe wa bunge maalumu kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa kudumu. |
|
Wajumbe wa bunge maalumu la katiba, Samuel Sitta na Andrew Chenge wakisalimiana wakati Mh Sitta akipiga kampeni za mwisho mwisho. |
Hatimaye ule mchakato wa kumpata mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalumu la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umetamati mara baada ya wajumbe wa bunge maalumu kumchagua Samuel John Sitta dhidi ya mpinzani wake, Hashim Rungwe.
Kampeni kutokea awali zilikuwa zikifanyika, huku mheshimiwa Samuel Sitta akisaidiana na mkewe, mheshimiwa Margret Sitta kugawa vipeperushi na kuwakumbusha watu uhitaji wao wa kura walipokuwa wanaanza kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa bunge maalumu.
Zifuatazo ni baadhi ya picha kama ambavyo GK imefanikiwa kuzinasa, baada ya kuweka kambi mjini Dodoma ili kukuhabarisha kinachojiri kwenye mchakato huu wa kupata katiba mpya kwa maendeleo ya taifa letu.
|
Wajumbe wa bunge maalumu la katiba wakiendelea na zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma. |
|
Mgombea, Mheshimiwa Hashim Rungwe akirejea kwenye nafasi yake mara baada ya kupiga kura. |
|
Mheshimiwa Samuel John Sitta akipiga kura kwenye uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa kudumu wa bunge maalumu la katiba |
No comments
Post a Comment