Writen by
sadataley
11:07 AM
-
0
Comments
Waziri mkuu wa China, Li
Keqiang, ameuambia mkutano wa kila mwaka, wa bunge la taifa hilo mjini
Beijing, kwamba maendeleo ya kiuchumi yanasalia kuwa jukumu kubwa zaidi
la serikali, lakini marekebisho ya kimsingi ni sharti yatekelezwa japo
ni machungu.
Bwana Li amewaambia maelfu ya wajumbe katika
bunge la taifa hilo, Great Hall of the People, kwamba shabaha ya kila
mwaka ya ukuaji wa kiuchumi itasalia kuwa asilimia saba nukta tano.Akizungumzia tatizo la uchafuzi, amesema kuwa moshi mkubwa unaondelea kutanda katika miji mikubwa ya China, ni onyo la kiasili dhidi ya maendeleo yasiokuwa na mpango.
Waziri huyo mkuu wa China kadhalika ametangaza marufuku dhidi ya majengo mapya ya serikali kama sehemu ya kile alichokitaja kuwa mapambano bila huruma dhidi ya ufisadi.
No comments
Post a Comment