Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, March 14, 2014

Japan haitabadili msamaha kwa watumwa

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema kuwa serikali yake haina nia kubadilisha msamaha wake kwa wanawake waliotumiwa kama watumwa wa ngono katika kambi za wanajeshi wa nchi hiyo wakati wa vita vya pili vya dunia na baada ya vita hivyo.
Sanamu ambayo ni ishara ya waliokuwa watumwa wa ngono Japan
Wanawake hao walilazimishwa kufanya kazi kama watumwa wa ngono katika madanguro ya wanajeshi
Wanajeshi wa Japan, waliwatumia maelfu ya wanawake wengi wao kutoka rasi ya Korea na nchini China kama watumwa wa ngono kati ya mwaka 1910 na 1945.
Wanasiasa kadhaa wazalendo, wanasisitizza kuwa hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa wanawake hao walilazimishwa na serikali au jeshi kujihusisha na kazi hiyo.
Lakini bwana Abe alisema kuwa hakuna mipango yoyote ya kuibadilisha msamaha wa mwanzo uliotolewa na serikali miaka kumi iliyopita kuwataka radhi wanawake hao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment