Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 13, 2014

CCM, Chadema waikaba NEC Iringa

Kalenga. Mvutano mkali umeibuka baina ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Vyama vya Siasa vya Chadema na CCM kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga kura Jimbo la Kalenga, baada ya kuonekana kuna wapiga kura 600 wa ziada.
Mvutano huo ulitokea jana mjini hapa, baada ya NEC kuitisha mkutano uliohusu maandalizi ya uchaguzi wa Jimbo la Kalenga, utakaofanyika Jumapili ijayo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alitaka ufafanuzi kwa Jaji Lubuva kuhusu Daftari hilo kufanyiw marekebisho bila wao kufahamu.
Mratibu wa Kampeni za CCM, Miraji Mtaturu aliomba wataalamu wa NEC na Chadema wakae ili kuona tatizo hilo na kwamba hata chama chake kinataka kifahamu kama kuna tatizo na limesababishwa na nini.
Naibu Katibu wa NEC na Mkuu wa Tehama, Dk Sisti Carial akijibu madai hayo alisema, wamefanya maboresho mwaka huu 2014 ili kuingiza majina ya watu ambao majina yao hayakuingizwa na wale ambao hawatakiwi kuwamo, wakiwemo marehemu.
Jaji Lubuva alihitimisha kwa kuwataka Chadema na wataalamu wa NEC kupata muda wa kueleweshwa vizuri suala hilo ili kuondoa wasiwasi.
Chadema pia walilalamikia suala la shahada za kupiga kura kuchukuliwa na wakala wa pembejeo, jambo ambalo linaweza kusababisha wapiga kura wengi kushindwa kuwachagua viongozi wanaowataka.
Msimamizi wa uchaguzi, Kisaka alisema atatoa agizo na matangazo kwa mawakala wote kuwarejeshea shahada zao ili kupiga kura siku hiyo ya uchaguzi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment