Writen by
sadataley
8:14 PM
-
0
Comments
Ilipofika saa 6:45 Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) walianza kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya, hali iliyosababisha wakazi hao kukimbilia kwenye nyumba zao.PICHA|MAKTABA
Mvomero. Wakazi wa Kijiji Melela Mangae, Kata ya Melela, wilayani Mvomero, wamefunga barabara ya Morogoro- Iringa kwa zaidi ya saa sita wakishinikiza kuondolewa kwa wafugaji wa jamii ya Kimasai kijijini hapo kwamba wamekuwa wakiwapiga na kuingiza mifugo mashambani.
Walianza kufunga barabara hiyo saa 3:00 asubuhi, huku wakazi hao wakisema baadhi ya wananchi sababu ya kufunga barabara hiyo ni kuchoshwa na wafugaji hao.
Walisema wamekuwa wakipeleka malalamiko yao kwa uongozi wa kata, lakini hakula linalofanyika.
Ilipofika saa 6:45 Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) walianza kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya, hali iliyosababisha wakazi hao kukimbilia kwenye nyumba zao.
Watu wanaokadiriwa kufika 48, wanawake wakionekana wengi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya uchochezi.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mvomero, Idd Ibrahim aliongza askari kuingia mtaani kuwasaka watuhumiwa na kufanikiwa kuwakamata 48.
No comments
Post a Comment