Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 13, 2014

Rais Panza aapa kukabiliana na waasi

Watu walioathirika na vita mjini Bangui
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza, ameapa kuwa atapambana na wapiganaji wa Kikristu ambao walihusika na mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya Waislamu katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Rais Samba-Panza amesema waasi hao, wanaojulikana kama, 'wanaopinga-balaka,' wamepoteza mwelekeo na hawana dhamira yoyote.
Maelfu ya Waislamu wameukimbia mji huo na kukimbilia nchi jirani ya Cameroon.Amesema wapiganaji hao ambao walikuwa watetezi wa jamii, wamegeuka na kuwa wauaji na waporaji.
Hata hivyo ushahidi wa mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Seleka unaendelea kutolewa.

Misikiti yabomolewa

Mwandishi wa BBC, mjini Bangui, Kassim Kayira, anasema kuwa, Waislamu wengi wamepiga kambi katika msikiti mkubwa zaidi nchini humo, baada ya misikiti mingine kuharibiwa, huku Wakristu nao wakipiga kambi karibu na uwanja mkuu wa Ndege.
Watu wakiwa kambini mjini Bangui
Aidha amesema hali katika kambi hiyo ni ya kusikitisha huku wakimbizi hao wa ndani wakihitaji misaada ya dharura kama vile vyakula na dawa.
Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty international limesema kinachotokea CAR ni kumalizwa kwa jamii.
Ripoti hiyo imetolewa wakati maelfu ya Waislamu wanaendelea kuukimbia mji mkuu Bangui wakielekea nchi jirani.

Wakati huo huo Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema ndege ya kwanza iliyosheheni misaada imewasili katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati Bangui.
Chanzo:bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment