Writen by
sadataley
12:53 PM
-
0
Comments
RISALA YA MAHAFALI YA KWANZA YA HUDUMA YA KUNUSURU
MAISHA YA MAMA NA MTOTO (CHILD SURVIVAL PROGRAMME)
Kituo cha huduma ya mtoto , PAG Mtwivila Student
Cenre kilianza tarehe 10 machi mwaka 2007.Kituo hiki ni miongoni mwa vituo vinavyofanya
huduma ya kumfungua mtoto kutoka katika maeneo ya umaskini wa kiroho,kiakili na
kijamii, kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la Compassion International. Katika
mkoa wa Iringa kuna vituo kumi na mbili vya huduma ya mtoto, miongoni mwa hivyo
vitatu vina huduma ya Child Survival Programme. CSP ni huduma ya kunusuru
maisha ya mama na mtoto.
PAG Mtwivila Student Center ni miongoni mwa vituo vyenye
huduma ya kunusuru maisha ya mama na mtoto. Kabla ya kuanzishwa huduma ya CSP
kituo kilikuwa tayari kimeanza na watoto 200 chini ya huduma nyingine
iliyotangulia ya CDSP kikiwa na watumishi wanne yaani; mkurugenzi, mhasibu, mtendakazi
wa jamii na mtendakazi wa afya. Huduma hii ya mama na mtoto ilianza Mei 2011
ikiwa na wamama 43 na watoto 26 na wengine
17 walizaliwa baada ya miezi michache kuandikishwa katika huduma hii. Kwasasa
tunao watoto 304 wakubwa na wadogo na wamama 40
katika huduma zote mbili kwa ujumla. Idadi ya watoto ambao kwa siku ya
leo tunawafanyia mahafali yao ya kufikisha miaka mitatu ni watoto kumi. Idadi
ya watoto tunawahudumia wapo katika makundi yafuatayo; watoto wadogo CSP ni 40,
shule ya msingi 241, sekondari 23 na chuo 1. Watoto hawa tunawapatia huduma
muhimu kama elimu huduma ya kiroho, mavazi, lishe na huduma ya afya.
Watoto hawa tumeona mafanikio na mabadiliko makubwa
ndani yao kiroho , kiakili, kimwili
tangu wakati walipoandikishwa mpaka kufikia sasa. Tunamshukuru sana Mungu kwa
kutoa shirika la kuwahudumia watoto pamoja na wachungaji wote waliokuwa tayari
kuonyesha ushirikiano katika huduma hii.
Katika huduma hii pia tunachangamoto ambazo
tunakabiliana nazo ni pamoja na kutokuwa na miundo mbinu ya kutosha ili kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi, kwasasa tunaendelea na ujenzi wa madarasa na kumalizia
ofisi.
Hii ndio risala yetu fupi Mwenyezi Mungu awabariki.
No comments
Post a Comment