Writen by
sadataley
3:56 PM
-
0
Comments
Alshabaab fighters
Ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Al-shabaab kutokana na ukiukwaji wa utaratibu katika serikali.
Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.
Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.
Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab.
No comments
Post a Comment