Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 11, 2014

Afueni kwa watuhumiwa wa Rwanda

Maelfu ya watu waliuawa wakati wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda
Mahakama maalum ya Kimataifa ya Rwanda- ICTR imefutilia mbali kesi dhidi ya maafisa waandamizi wawili watuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda.
Uamuzi huu umetolewa katika kesi yao ya rufaa.
Walishitakiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, ambayo inakadiriwa watu laki nane walipoteza maisha.
Aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Augustin Ndindiliyimana, ameelezewa kama mmoja wa watu wa ngazi ya juu waliohukumiwa na mahakama hiyo inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Afisa wa pili, Francois-Xavier Nzuwonemeye alikuwa kamanda msomi wa kikosi cha jeshi.
Mahakama ya ICTR pia imepunguza muda wa kifungo cha afisa wa tatu.
Hata hivyo uamuzi kuhusu rufaa ya mkuu wa zamani wa Jeshi Augustin Bizimungu haujatangazwa bado.
Chanzo: bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment