Writen by
sadataley
6:58 PM
-
0
Comments
Mzozo wa Sudan Kusini wapata sura mpya
Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek Machar katika picha.
Kiongozi wa waasi wa sudan kusini Riek Machar amesema upande wake hauko karibu tena kufikia makubaliano ya amani kufuatia mkutano wake na wapatanishi wa afrika jumamosi.Wapatanishi kutoka eneo la Afrika mashariki- IGAD walikutana na bwana Machar katika eneo la siri huko Sudan kusini.
Akizungumza na sauti ya amerika kwa njia ya simu jana , Machar alionesha matumaini madogo ya kuwepo na upatanishi wa kumaliza mzozo wa mapigano uliodumu kwa karibu mwezi mmoja sasa nchini Sudan.
Anasema jambo muhimu ni kuendelea kushikiliwa wafungwa 11 wa kisiasa wa upinzani ambao walikamatwa mapema wakati mzozo huo ulipozuka pamoja na taarifa kwamba jeshi la Uganda linaunga mkono vikosi vya serikali ya Sudan kusini.
Kufuatia mkutano wiki iliyopita na rais wa sudan kusini Salva Kiir na wafungwa wa kisiasa , ujumbe wa IGAD ulisema kwamba wafungwa walidai kuwa kushikiliwa kwao isiwe ndio kichochea cha kufikia makubaliano.
Uganda pia ilikanusha tuhuma kwamba majeshi yake yanahusika katika ghasia na kusema kwamba vikosi vyake vipo nchini humo ili kulinda raia wa Uganda.
Maafisa wa serikali ya Sudan kusini wamesema wapatanishi wa IGAD wamerejea Addis Ababa ambako mazungumzo ya amani yanatarajiwa kufanyika.
Machar amesema kundi lake litaendelea kuhusika na mashauriano katika mji mkuu wa Ethiopia kwa lengo la kumaliza ghasia.
No comments
Post a Comment