Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 15, 2014

Msani wa Kenya ang'ara Hollywood

kutoka kushoto Lupita Nyong'o, Chiwetel Ejiofor, Steve McQueen, Sarah Paulson, na Michael Fassbender katika picha kwenye tuzo za Golden Globe.
kutoka kushoto Lupita Nyong'o, Chiwetel Ejiofor, Steve McQueen, Sarah Paulson, na Michael Fassbender katika picha kwenye tuzo za Golden Globe.
Mcheza sinema Lupita Nyong’o kutoka Kenya alikuwa mmoja wa wanawake waliong’ara katika sherehe za tuzo za Golden Globe kwa wacheza sinema huko Hollywood, California. Lupita alishiriki katika sinema ya “12 Years a Slave” ambayo ilikuwa moja ya sinema zilizojizolea tuzo nyingi katika sherehe za Jumapili usiku, ikiwa ni pamoja na sinema bora katika aina ya drama.

Lupita ambaye alianza kujulikana zaidi Afrika katika mfululizo wa tamthiliya ya MTV Shuga, Kenya, alicheza kama msichana mtumwa katika sinema ya “12 Years a Slave.”

Jumapili alitokeza akiwa amevalia gauni refu jekundu na kutajwa kama miongoni mwa wanawake waliopendeza sana katika sherehe hizo.

Sinema ya “ 12 Years a Slave” iliyoongozwa na mkurugenzi Steve McQueen inaelezea jinsi mwanaume mmoja mweusi alivyotekwa na kuuzwa kama mtumwa kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani.

Pia mtengenezaji wa filamu kutoka Mexico, Alfonso Cuaron alitajwa kama mwongozaji mahiri katika utengenezaji wa sinema za drama. 

Wengine waliotamba katika tuzo za Golden Globe ni pamoja na mcheza sinema Mathew McConaughey aliyepata tuzo yake kwa kuwa muigizaji bora katika mitindo ya drama za hisia kwenye filamu ya “Dallas Buyers Club” na Leonardo DiCaprio alipata tuzo bora akijulikana sana katika drama kwenye muziki au uchekeshaji, filamu iliyompa chati ni “ The Wolf of Wall Street”.

Tuzo za Golden Globe ni mfululizo wa kipindi cha tuzo za Hollywood ambazo kilele chake kitakuwa tuzo maarufu zinazojulikana sana kama Oscars Machi  mbili.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment