Writen by
sadataley
6:42 PM
-
0
Comments
Na Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa uamuzi, dhidi pingamizi zilizowasilishwa na upande wa mlalamikiwa kwa njia ya maandishi dhidi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kinana anamtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, kufuta matamshi ya kumkashifu, kumfedhehesha na kumhusisha na ujangili wa meno ya tembo.
Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Zainabu Muruke, baada ya Mchungaji Msigwa kupitia wakili wake, Peter Kibatala kuwasilisha kwa njia ya maandishi, pingamizi lake dhidi ya mlalamikaji ambapo anaiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kwa madai kuwa ina upungufu kisheria.
Kwa mujibu wa Msigwa kupitia wakili wake Kibatala wanadai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na Kinana dhidi yake, haina mashiko kwa sababu ilikosewa jinsi ya kufunguliwa.
Walidai kuwa kesi hiyo ilikosewa namna ilivyofunguliwa Ilipaswa kufunguliwa mkoani Mwanza ambapo tukio linadaiwa kutokea ama mkoani Iringa kwenye makazi ya kudumu ya Mchungaji Msigwa. Hivyo wanaiomba mahakama kuifuta kwa sababu ina upungufu wa kisheria.
Kinana anaiomba mahakama iamuru Mchugaji Msigwa amlipe kiasi cha Sh 350 milioni kutokana na matamshi ya Aprili 21, 2013, yaliyotolewa katika mkutano wa hadhara.
No comments
Post a Comment