Writen by
sadataley
10:01 PM
-
0
Comments
Na Aidan Mhando, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, ameongoza viongozi wa Serikali na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa msajili wa kwanza wa vyama vya siasa nchini, Jaji George Liundi, katika Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Mbali na Rais Kikwete viongozi wengine waliyoshiriki kuaga mwili wa Jaji Liundi ni Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib na Rais mstaafu Benjamini Mkapa.
Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwenyekitiwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Ofisi ya vyama vya siasa iliwakilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa mstaafu, John Tendwa, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa akiwamo Profesa Ibrahimu Lipumba wa Chama Cha Wananchi CUF na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
Baada ya taratibu za kuaga mwili wa Jaji Liundi, alizikwa jana kwenye makaburi ya Chang’ombe Maduka Mawili ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick aliongoza maziko hayo.
Kauli ya Serikali
Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetumikia serikali kwa muda mrefu kuanzia mwaka 1966.
Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetumikia serikali kwa muda mrefu kuanzia mwaka 1966.
Mbali na hilo, Lukuvi alisema historia inasema Jaji Liundi ndiye Mtanzania wa kwanza kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha na alisaidia kutengeneza Katiba ya sasa, kwa kutafsiri baadhi ya vifungu ambavyo vilitoholewa kutoka kwa wakoloni .
Vyama vya siasa
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Dk Emmanuel Makaidi akizungumza kwa niaba ya vyama vya siasa vyenye usajili alisema, Jaji Liundi alikuwa kiongozi na mtumishi wa serikali ambaye hakupenda makuu.
Makaidi alisema ni viongozi wachache nchini wenye sifa kama alizokuwa nazo Jaji Liundi, “Alikuwa na cheo kikubwa lakini maisha yake hayakutofautiana na watu wa kawaida.
No comments
Post a Comment