Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, January 20, 2014

Baraza la mawaziri labadilishwa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kuwateua mawaziri na manaibu waziri, kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki dunia hivi karibuni.
Rais Jakaya Kiwete wa Tanzania
Katika uteuzi huo Rais Kikwete amewateua mawaziri wapya wawili na manaibu waziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo manaibu waziri wanne kuwa mawaziri kamili.
Miongoni mwa mawaziri wapya ni pamoja na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dokta Asha-rose Migiro, ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria, huku Dk. Titus Kamani akiteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri pekee aliyeachwa katika mabadiliko hayo ni aliyekuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa.
Miongoni mwa manaibu waziri wapya ni pamoja na Juma Nkamia ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtangazaji, ambaye amepewa dhamana katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete yametokana na kujaza nafasi za mawaziri ambao walilazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya bunge kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili kubaini kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utesaji na udhalilishaji vikidaiwa kutendwa na watekelezaji wa operesheni hiyo.
Ripoti hiyo iliwalazimisha waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutangaza kujiuzulu, huku naye waziri wa mambo ya ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi kufuata mkondo huo bila kumwaacha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha, na Dr.
Mathayo David Mathayo aliyekuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kutokana na wizara zao kuhusika katika usimamizi wa operesheni hiyo ambayo iliwahusisha polisi, askari jeshi na walizni wa wanyamapori.
Huku nafasi ya tano katika baraza hilo ikiachwa wazi na aliyekuwa waziri wa fedha, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.

Tanzania yaomboleza kifo cha Komla Dumor.

Katibu Mkuu Kiongozi katika serikali ya Tanzania, Balozi Ombeni Sefue, ambaye ndiye aliyetangaza mabadiliko ya baraza hilo la mawaziri, pia alitumia fursa hiyo kutoa salaaam za pole kwa Shirika la Utangazaji la BBC kutokana na kifo cha ghafla cha mtangazaji wake maarufu wa Televisheni na Redio, Komla Dumor, ambapo alimwelezea kuwa mtangazaji ambaye alifanya kazi yake kwa weledi mkubwa na hivyo kulijengea heshima bara la Afrika.
"nianze kutoa pole kwenu na kwa taaluma yenu kwa msiba wa Komla Dumor. Kama mnavyomfahamu alikuwa mtangazaji maarufu wa BBC na kwetu sisi waafrika ni jambo la faraja inapokuwa kwamba habari za Afrika zinatangazwa na mwaafrika. Bwana Komla Dumor amefanya kazi nzuri sana, ni wazi kabisa hakupewa nafasi ile kwa sababu tu ni mwaafrika lakini na uwezo wake ulikuwa mkubwa sana, kwa hiyo aliipa Afrika heshima kubwa sana. Na katika kipindi hiki cha majonzi kwa kweli naunga nanyi katika kupeleka salaam zetu za rambirambi kwa familia yake, kwa BBC na kwa waafrika wote na Ghana kule alikotoka, kwamba msiba huu ni wetu sote Afrika." alisema Balozi Sefue.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment