Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, January 18, 2014

BAADA YA KAZI NZITO 2013, KWETU PAZURI WAPONGEZANA


Sarah Uwera mmoja kati ya solo hodari wa Ambassadors akiwa katika pozi.
Baada ya kazi nzito ya utumishi waliyoifanya mwaka jana, kwaya ya mabalozi wa Yesu ama waite Ambassadors of Christ wanaofahamika zaidi kwa album yao ya Kwetu Pazuri kutoka nchini Rwanda, waliamua kuwa na siku ya kipekee kwa wanakwaya wote kwenda ufukweni kupongezana kwa kazi ya kumuhubiri Kristo wanayoifanya.

Katika pikiniki yao iliyofanyika ufukwe wa Rwesero huko nchini kwao, walishinda pamoja wakipeana shuhuda, kula pamoja, michezo pamoja na uimbaji ambapo uongozi wa kwaya hiyo uliwapa vyeti vya heshima baadhi ya wanakwaya wa kwaya hiyo kwa utumishi wao wa kumuhubiri Kristo kupitia kwaya hiyo. Ambapo pia kwaya hiyo ilitumia muda huo kutiana moyo wanakwaya wote tayari kwa kumtangaza Kristo kwa mwaka 2014

Twendeni mabalozi tukapunge upepo.
Mandhari saaafi.
Picha ya pamojaaa.

Sijajua haya matofali yanawekwa chiniii ama yanataka kurushwa mwe!
Soka ilichezeka haswa bila kujali jua.
Soka pia walicheza.
Karata zilikuwepoo.
Hata hii walichezaaa.
Moja ya kitambulisho cha Ambassadors.
Msosi ulikuwepo.
Waimbaji wakiwa bize kupiga stori.
Flora naye akakumbukwa kwa utumishi wake.
Mwanadada Getrude akipokea cheti chake kwa utumishi mwema ndani ya kwaya hiyo. ©KJ Marcello Velsco.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment