Writen by
sadataley
10:12 PM
-
0
Comments
DUNIA YOTE YATUA UWANJA WA FNB SOWETO
Joyous Celebration na Soweto Gospel Choir ni kati ya makundi yaliyotarajiwa kuimba siku ya leo wakati wa ibada maalumu ya kitaifa kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Afrika ya kusini marehemu Nelson Mandela inayotarajiwa kufanyika katika uwanja wa FNB uliopo Soweto nchini Afrika ya kusini.
Ibada hiyo maalumu inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali mashuhuri duniani wakiwemo marais Barack Obama wa Marekani atakayeambatana na marais waliomtangulia Bill Clinton pamoja na George W Bush, Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ambaye naye ataambatana na mawaziri wakuu waliomtangulia Gordon Brown, Tony Blair pamoja na Sir John Mayor huku malkia Elizabeth atawakilishwa na mwanae Prince Charles.
Ukiachana na viongozi hao pia marais kutoka nchi mbalimbali pamoja na viongozi wengine wanatarajiwa kuhudhuria hii leo katika tukio ambalo linatarajiwa kuanza majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika ya kusini. Joyous kwa upande wao walikuwa na zoezi kali jana mpaka majira ya saa 2 za usiku wakijiandaa na tukio hilo huku upande wa Soweto Gospel Choir kwaya iliyopo Afrika ya kusini ndiyo itakayowakilisha huku kundi lingine likiwa bado barani ulaya kwa ziara yao ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
![]() |
| Baadhi ya waimbaji wa Joyous Celebration katika moja ya huduma zao. |



No comments
Post a Comment