Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, October 21, 2013

Wanafunzi wapambana na polisi Cairo

Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.Mapambano mjini Cairo
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment