Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, October 16, 2013

Wakuu wa Vyama vya upinzani Tanzania waridhishwa na mazungumzo yao na Raisi Kikwete

Wakuu wa Vyama vya Upinzani nchini Tanzania muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yao na raisi Kikwete
Wakuu wa Vyama vya Upinzani nchini Tanzania muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yao na raisi Kikwete
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania, wameeleza kuridhishwa na mazungumzo waliyofanya na rais Jakaya Kikwete,kuhusu marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba na kwamba watawasilisha maoni yao kwa vyombo husika.
Kwenye mazungumzo hayo, viongozi wa upinzani walikuwa na madai mbalimbali ikiwemo kutoridhishwa na hatua ya wabunge wa chama tawala CCM kupitisha muswada huo bila ya muafaka na upinzani bungeni pamoja na kutaka kufanyika marekebisho kwenye sheria hiyo kabla ya kutiwa saini na rais.
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ni mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF na alihudhuria mazungumzo hayo ikulu jijini Dar es Salaam katika mahojiano maamul na rfikiswahili alibainisha kuwa mazungumzo yana dalili za kheri na kufanikiwa kwa mpango huo kwakuwa raisi ameunga mkono jitihada hizo kuhusisha wanaharakati na wadau mbamlimbali nchini Tanzania.
Rais Kikwete amevitaka vyama hivyo kuwasilisha maoni ya mapendekezo yao Serikalini ili yashughulikiwe pamoja na kuwepo kwa mfumo wa mawasiliano kati ya vyama vya siasa na serikali kama wadau muhimu wa kuhakikisha katiba bora inapatikana.
Mazungumzo hayo yanakuja ikiwa ni majuma kadhaa kupita ambapo vyama vya upinzani nchini Tanzania viliungana na kufanya mkutano wa pamoja kuwarai wananchi kuungana pamoja kumtaka raisi kutotia saini sheria hiyo ya muswada wa katiba mpya hatua mabayo imekuwa ikiungwa mkono na chama Tawala bungeni CCM.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment