Writen by
sadataley
6:13 AM
-
0
Comments
Rais wa Ufaransa François Hollande na mwenyei wake wa Afrika Kusini Jacob Zuma,jijini Pretoria, Octoba 14. 2013.
Rais wa Ufaransa François Hollande na mwenyei wake wa Afrika Kusini Jacob Zuma,jijini Pretoria, Octoba 14. 2013.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amewasili leo jumatatu Octoba 14 mwaka 2013, jijini Pretoria ikiwa ni ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini akiambatana na ujumbe wa mawaziri wanane wa serikali yake pamoja na matajiri zaidi ya ishirini. Ziara hiyo inajiri takriban miaka ishirini baada ya ile ya rais mwengine wa Ufaransa kutoka chama cha kisocialist Francois Mitterand mwaka 1994 na alipokelewa na rais Nelson Mandela zama hizo.
Ziara hiyo imeanza mchana kwa mkutano wa pamoja wa ma rais Francois Hollande na mwenyeji wake Jacob Zuma na vyombo vya habari. Francois Hollande ameweka wazi hisia zake baada ya kuzuru taifa hilo kwa mara ya kwanza.
Kwa pande zote mbili inaonyeha ni kiasi gani uhusiano baina ya mataifa haya mawili umeanza kurejea baada ya kutofautiana kuhusu Libya na Cote d'Ivoire.
Kuna baadhi ya mvutano kati ya nchi hizi mbili katika Afrika. Hususan kuhusu mzozo wa jamhuri ya Afrika ya kati ambapo nchi hizi zimetofautiana sana kuhusu hali ya mambo.
Viongozi hawa Jacob Zuma na rais Hollande wametumia fursa ya mkutano wao huu wa pamoja ili kuondowa tofauti zao kuhusu mzozo wa jamuhuri ya Afrika ya kati na kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja kutafuta suluhu ya mzozo uliopo nchini humo kupitia taasisi za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Ufaransa itasaidia kuongeza nguvu vikosi vya Jumuiya ya kikanda vitavyopelekwa huko.
kutumika mkutano wao wa chuma nje tofauti zao na kukubaliana kufanya kazi pamoja ndani ya mfumo wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Ufaransa, kama sisi kujua, kusaidia kanda ya Afrika nguvu kwamba utatekelezwa.
Akizungumza na vyombo vya habari rasi Hollande amesema Ufaransa haipo kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya waafrika, lakini ipo kwa ajili ya kuongozana. Na hii ndio kauli ya rais Hollande aliyo itowa wakati wa hotuba yake jijini Dakar mwaka uliopita. Ufaransa haitaki kuwa polisi ya Afrika.
Rais huyo amefahamisha kuwa rais Jacob Zuma atahudhuria katika mkutano wa kilele mjini Paris mwezi Desemba, utaojadili kuhusu Usalama katika bara la Afrika na maendeleo yaliofikiwa katika mchakato wa kuunda kikosi cha kuingilia kati mizozo.
Ziara hiyo inaangaliwa pia katika nyanja ya kibiashara. Mikataba kadhaa imetiwa saini. Rais wa Ufaransa ametangaza wa Ufaransa ametangaza kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa mafuta wenye uwezo wa Euro bilioni 1.5.
Viongozi hao wawili pia wameithibitisha pia mkataba wa reli uliosainiwa mwaka jana. Kiwanda cha Alstom kitatowa mabehewa ya treni 3600 nchini Afrika Kusini. Viwanda vitakuwa nchini Afrika Kusini, Ufaransa itatowa mafunzo kwa wataalamu wake.
No comments
Post a Comment