Writen by
sadataley
10:30 AM
-
0
Comments
Umoja wa Mataifa UN umelituhumu kundi la waasi la M23 kuwa chanzo cha kuvunjika kwa mazugumzo ya amani kati yake na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yaliyokuwa yakiendelea jijini Kampala nchini Uganda.
Umoja wa Mataifa UN umekuwa ukishinikiza kupatikana kwa suluhu la kudumu kati ya waasi hao na serikali ya Kinshasa ili kurejesha amani Mashariki mwa nchi hiyo.
Hata hivyo kundi hilo limekuwa likitupia lawama wajumbe wa serikali waliomtaka Naibu kiongozi wa ujumbe wa waasi wa M23 Roger Lumbala kujiondoa katika mazungumzo hayo.
Aidha Lumbala amerejesha lawama kwa upande wa Serikali kupitia wajumbe wake kwa kuona wamedharau M23 na haoni kwanini wajumbe wamejiondoa katika mazungumzo hayo wakati walikuwa karibu kupata muafaka.
Marekani nayo kwa upande wake imeeleza kusikitishwa na hatua ya kuahirishwa kwa mazungumzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea kuanzia mwezi uliopita.
Pande zote mbili zilitangaza kusitisha mazungumzo hayo ya amani yaliyokuwa yakiendelea mjini Kampala nchini Uganda muda mfupi baada ya mjumbe wa Umoja wa mataifa kuonya juu ya hatari itakayotokea ikiwa mpango wa makubaliano hautafikiwa mara moja kukomesha mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Wajumbe maalum wa Umoja wa Mataif UN waliarifu mapema jumatatu kuhusu kukosekana kwa mpango wa msingi wenye lengo la kukomesha mapigano yanayosababishwa na kundi hili la waasi wa m23 ambao wamesababisha hali ya sintofahamu katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini.
No comments
Post a Comment