Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, October 20, 2013

Daftari la wapigakura kuanza kuboreshwa

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema, Mchakato wa Kuboresha daftari la kudumu la wapigakura uko katika hatua za mwisho.
Jaji Lubuva akizungumza na gazeti hili alisema, wanachokifanya sasa ni kuandaa vitendea kazi na kuangalia vituo vya kupigia kura vilivyotumika mwaka 2010 kama bado vipo.
“Naweza kusema tuko katika hatua nzuri na hivi karibuni tutaanza kuriboresha daftari hili ili waliotimiza miaka 18 wanaingizwa na kuyaondoa majina ambayo wahusika wamepoteza sifa za kuwamo,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema mchakato huo wa kuriboresha daftari hilo utafanyika mapema iwezekanavyo kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya kuipitisha Katika Mpya.
Jaji Lubuva alisema hatua za kuliboresha daftari hilo unawahusisha wadau mbalimbali wakiwamo vyama vya siasa ili kuhakikisha mchakato huo unafanikiwa kwa ufanisi.
Suala la kuboreshwa Daftari la Wapigakura limekuwa likipigiwa kelele sana na wanasiasa wakitaka suala hilo lifanywe mapema ili watu ambao hawakuandikishwa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wapate fursa ya kupiga kura.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment