Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, October 14, 2013

AU yataka ICC iahirishe kesi ya Kenyatta

Rais Kenyatta akiwa katika mahakama ya ICC.

Rais Kenyatta anakabiliwa na kesi inayoanza kusikilizwa mwezi Novemba.
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia umetaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) huko The Hague icheleweshe kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa Novemba mwaka huu.AU pia wamekubaliana azimio linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la Afrika aliyeko madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC.
Kucheleweshwa
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment