Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, October 13, 2013

AU yapitisha azimio kuhusu ICC

Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya asihudhurie kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ila ikiwa itaakhirishwa.Kikao cha AU
Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema kuwa kiongozi yeyote wa taifa asitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani
Kesi ya Rais Kenyatta ambaye anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu inatarajiwa kuanza mwezi ujao mjini Hague, ingawa ameomba mara kadha kwamba iakhirishwe.
Bwana Kenyatta siku zote amesema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.
AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, alisema kesi za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar al-Bashir wa Sudan zinaweza kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano katika nchi zao.
Mkutano umemalizika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment