Writen by
sadataley
10:20 PM
-
0
Comments
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.Zoezi la kuwahamisha wahamiaji haramu kutoka nchini Tanzania ambalo limekuwa likiendelea kwa wiki kadhaa sasa linachukua sura nyingine baada ya baadhi ya watu hao wanaohamishwa kudai ni Watanzania halisi wanaolazimishwa kupelekwa kwa nguvu katika nchi jirani.Vilevile wengine wanasema maafisa wa uhamiaji na maaskari wanaoendesha operesheni hiyo wamewajeruhi na kuwachomea nyumba zao.
Baadhi ya nchi zinazowapokea watu hao ni pamoja na Rwanda ambayo mpaka sasa imekwishawapokea wapatao elfu saba na mamia kadhaa ya mifugo.
Pamoja na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kuomba zoezi hilo liendeshwe kwa uangalifu taarifa zinazotolewa na watu hao zinadai kwamba wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kama vile kujeruhiwa,kuchomewa nyumba na kunyang'anywa mali zao.
Lakini zaidi ya hayo kuna wengine waliokutwa katika eneo la Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda wanaodai kwamba ni Watanzania halisi ambao walifurushwa na maafisa wa usalama.
Nayo wizara ya mambo ya ndani kupitia mseji wake bwana Isack Nmtanga imekanusha juu ya taarifa hizo na kusema kuwa muda halisi ulitolewa kwa wahamiaji haramu kuondoka kwa hiari yao.
Amesema kuna vigezo kadhaa vinavyozingatiwa wakati wa kuwarejesha wahamiaji haramu katika nchi jirani na hakuna malalamiko yoyote waliyopata kuhusu shutuma za manyanyaso, kuporwa mali zao au hata kuchomewa nyumba zao.
No comments
Post a Comment